De Letras a Canción Generador de Letras Precios Mis Canciones

Nimekupatia

Song generated By ✨LyricsintoSong.com

Song Cover
v1

@ Johny Mgaya

2026-06-13 19:57:40

Letras

Chorus
Nimekupatia moyo wangu kama zawadi yako, ufanyie chochote ambacho unataka kuufanyia lakini usiuvunje.
Verse 1
Kila dakika ninayochukua nikiwa na wewe huwa ni spesho. Tunagawa hisia zetu na maisha yetu pamoja. Hivyo napenda zile hisia zote, ambazo tunakuwa nazo wakati huo. Nakupenda mpenzi wangu.
Nikikuweka mikononi mwangu, nahisi amani ikizunguka katika kumbato letu. Nakupenda na utakuwa karibu yangu kila wakati.
Maneno hayaji kirahisi, lakini ninapokuwa na wewe, moyo wangu unadunda kwa haraka, na nyota zinang'aa zaidi.
Chorus
Nimekupatia moyo wangu kama zawadi yako, ufanyie chochote ambacho unataka kuufanyia lakini usiuvunje.
Verse 2
Kila kitu kimekamilika katika dunia yangu, hii ni kwa sababu ya penzi letu ambalo tunagawa.
Kila nikifunga macho yangu, huwa nakuona mbele yangu. Kutengana kimwili hakuwezi kuzuia penzi letu, ambalo tunalithamini tangu jadi.
Haijalishi mahali popote ulipo, kwa kuwa mara kwa mara, unakuwa ndani ya moyo wangu na fikra zangu.
Chorus
Nimekupatia moyo wangu kama zawadi yako, ufanyie chochote ambacho unataka kuufanyia lakini usiuvunje.
Verse 3
Siku yangu huanza kwa kukufikiria wewe mpenzi wangu, na huishia hivyo hivyo.
Nakupenda wangu laazizi.
Kama ningepewa nichague kati ya kulia na wewe, ama kutabasamu na mwingine, ningekuchagua wewe kila wakati. Wewe ni penzi la maisha yangu.
Wewe ni zaidi ya mwanamke bora kwangu, wewe ni kila kitu kwangu. Nakupenda kwa moyo wangu wote.
Chorus
Nimekupatia moyo wangu kama zawadi yako, ufanyie chochote ambacho unataka kuufanyia lakini usiuvunje.
Verse 4
Laazizi wangu, wewe ni zaidi ya mchumba wangu, kila siku ni wewe unayeleta furaha ndani yangu, siku baada ya siku.
Wewe ni chuma katika ngao yangu, upepo katika dau langu, na mdundo katika moyo wangu.
Kwa mahabuba wangu, mpenzi wangu ninayempenda, tumekamilika tukiwa pamoja. Asante, kwa kugawa maisha yako na mimi.
Natamani niwe kitu cha kwanza ambacho unafikiria, pindi unapoamka mpenzi wangu.
Itakuwa fahari yangu iwapo nitakuwa mtu wa mwisho, kumfikiria kabla hujaenda kulala.
Chorus
Nimekupatia moyo wangu kama zawadi yako, ufanyie chochote ambacho unataka kuufanyia lakini usiuvunje.

Estilo de Música

Classical, danceable beat, male vocal